KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, July 10, 2010

UN yalaani shambulizi la manuari ya Korea
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani shambulizi dhidi ya manuari ya kijeshi ya Korea ya Kusini ambapo watu 46 waliokuwemo waliuwawa.
Meli iliyozama ya Korea Kusini

Meli iliyozama ya Korea Kusini

Taarifa hiyo ilisita kutaja Korea ya Kaskazini, licha ya matokeo ya uchunguiz wa kimataifa kugundua kuwa utawala wa Pyongyang ulihusika.

Katika uamuzi huo Baraza la Usalama lilijihakikishia uungwaji mkono kutoka kwa mshirika mkubwa na mwenye nguvu wa Korea ya Kaskazini, Uchina, ili kuonyesha Umoja katika baraza.

Pia lilijiepusha kuutenga zaidi utawala wa Pyongyang,na inatarajia kuishawishi nchi hiyo kurejea katika mazungumzo ya pande sita yanayolenga kusitishwa kwa mpango wa nuclear wa taifa hilo.

Balozi wa Korea ya Kaskazini katika Umoja wa Mataifa aliunga mkono azimio hilo, kwa kusema ni ushindi mkubwa wa kidiplomasia kwa nchi yake.

Marekani na Korea ya Kusini zilitaka Korea ya Kaskazini ilaaniwe moja kwa moja kutokana na shambulizi hilo.

Lakini mabalozi wao walipokea vema taarifa hiyo, na kusema inatuma ujumbe wa kimataifa uliowazi kwa Pyongyang, huku waelezea kuwa neno "shambulizi" si neno linaloashiria kutounga mkono upande wowote.

No comments:

Post a Comment