KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 10, 2010

Padri wa Rwanda akana mashtaka


Padri kutoka Rwanda aliyekamatwa wiki iliyopita na kushutumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 amekana mashtaka katika mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Jean-Bosco Uwinkindi alikamatwa baada ya kuingia magharibi mwa Uganda akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Anashutumiwa kwa kuamuru mauaji ya Watutsi baada ya watu hao kuomba hifadhi katika kanisa lake.

Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuliwa na wapiganaji wa Kihutu katika mauaji ya kimbari yaliyodumu kwa siku 100.

Bw Uwinkindi alifunguliwa mashtaka na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICTR) mwaka 2001, iliyopo Tanzania, kwa makosa ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu.

Mashtaka hayo yalisema padri huyo alikuwa wa kanisa la Pentekosti karibu na mji mkuu wa Rwanda, Kigali, mwaka 1994.

Upande wa mashtaka unadai uchunguzi uliofanywa baada ya mauaji hayo yalishuhudia takriban maiti 2,000 za watu karibu na kanisa hilo.

Hadi alipokamatwa na polisi wa Uganda, Bw Uwinkindi alikuwa miongoni mwa washukiwa 11 waliokuwa wakisakwa na ICTR.

Marekani ilitangaza kutoa zawadi ya dola za kimarekani milioni 5 kwa taarifa yeyote itakayosababisha kukamatwa kwa Bw Uwinkindi.

No comments:

Post a Comment