KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, July 26, 2010

Pakistan yakanusha kuwasaidia Taliban

Pakistan imekanusha vikali madai kuwa maafisa wake wa kijasusi wamekuwa wakiunga mkono wanamgambo wa Taleban nchini Afghanistan. Rais wa Pakistan amesema madai hayo hayana msingi.

Msemaji wa Rais wa Pakistan, Bi Farah Nazi Ispahani, amesema hatua ya kufichua siri hizo huenda ikawa ni jaribio la kuhujumu majadiliano ya mkakati mpya baina ya Marekani na Pakistan.

Magazeti ya Marekani ambayo huchapishwa nchini Uingereza, Marekani na Ujerumani yana taarifa kuwa maafisa wa ujasusi wa Afghanistan waliwasaidia wanamgambo wa Taliban kupanga mashambulio dhidi ya majeshi ya NATO, Umoja wa Mataifa na maeneo kadhaa nchini India.

Mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi ya Pakistan, Luteni Jenerali Hamid Gul, pia amekanusha madai hayo.

Nyaraka

Zaidi ya nyaraka 90,000 za kisiri za jeshi la marekani zimechapishwa katika mtandao mmoja Wikileaks. Nyaraka hizo zimetoa habari za siri kuhusu vita vya Afghanistan.

Kabla ya kuchapishwa kwa nyaraka hizo, gazeti la The Guardian na mengine mawili yalikuwa yameshaziona.

Nyaraka hizo zimeonyesha jinsi wanajeshi wa kimataifa walivyowaua raia nchini afghanistan na pia imedhihirisha kuwa kundi la Taliban linamiliki makombora ya kulipua ndege.

Kujitokeza kwa taarifa hizo ambazo zilikuwa za siri ni tatizo kubwa kwa utawala wa Obama. Kwa jumla, maswala mengi yanajulikana, hii ni pamoja na kushuku kuwepo kwa uhusiano kati ya majasusi wa Pakistan na wanamgambo wa Afghanistan.

Ujasusi

Ni vigumu kujua uzito wa kila taarifa. Lakini inaonyesha kuwa maafisa wa Marekani hawakuonesha nia ya kuchukulia kwa uzito wasiwasi kuhusu uhusiano wa Pakistan na Taliban pamoja na masuala mengine muhimu, ikiwemo uwezo wa wanamgambo.

Nyaraka hizi pia zimetokea wakati Marekani na washirika wake wengine wakijaribu kutafutwa kuungwa mkono kwa mikakati yake ya Afghanistan,lakini pia kuna upinzani mkali na maswali mengi yameibuka mjini Washington na miji mengine mikuu.

Pia ni wakati ambapo utawala wa Obama umejaribu kuangalia tena upya mikakati yake ya Pakistan kwa kile kilichokuja kujulikana kama mikakati ya Af-Pak.

Kuonekana kwa taarifa hizi bado ni kitendawili kwa uhusiano wa Marekani na serikali ya Pakistan, serikali ya Afghanistan na kwa hakika washirika wa Marekani, pamoja na maswali mengi juu ya namna gani nyaraka muhimu kama hizi zinaweza kujulikana na watu ambao wasiopaswa kujua.

No comments:

Post a Comment