KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 1, 2010

Ndege ya jeshi yaanguka Tanga, marubani wawili wafa papohapo


NDEGE ya kivita ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) kikosi cha Ngerengere mkoani Morogoro imeanguka wakati ipo katika mazoezi huko Mkoani Tanga jana,
Ndege hiyo ilikuwa na marubani wawili waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi walifariki mara baada ya ndege hiyo kuanguka na kugongana na lori.

Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 3.45 asubuhi, katika Kijiji cha Manga, Kata ya Mkata, wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga, Bw. Libaratus Sabas, alisema kuwa ndege hiyo ilianguka katikati ya barabara kuu ya Tanga Chalinze na kuserereka na kugongana na lori lenye namba F 6980 FH, Benz lililokuwa limebeba watalii 19.

Alisema lori hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Simon Mucheni (45), raia wa nchini Kenya wakielekea Dar es Salaam na kugongwa na ndege japo alijitahidi kuikwepa ndege hiyo na kuja kugongwa ubavuni mwa lori hilo na kuanguka.

Alisema watalii wote waliokuwa katika gari hilo walinusurika na kutoka salama.
Alisema wanajeshi hao waliweza kupata ajali kwa kile alichodai kuwa rubani Meja Cuthbert alikuwa akimfundisha Luteni Andrew na ndege hiyo baadae ikapata hitilafu na kuanguka.

Wanajeshi walioweza kupoteza maisha ni Meja Cuthbert Leguna (41) na Luteni Andrew Kijangi (31), wote wa Kikosi cha Jeshi Ngerengere mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment