KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 1, 2010

Kichanga chatumbukizwa chooni


MAITI ya mtoto mchanga imekutwa imetumbukizwa chooni huko maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, ilisema kuwa, maiti hiyo ilikutwa ikiwa imetupwa katika choo cha Ronwadi Mwaraku eneo hilo bila mwenyewe kutambua.

Alisema kichanga hicho kinakadiliwa kuwa na umri wa siku moja au mbili na mtu aliyehusika kufanya kitendo hicho hakufahamika mara moja.

Alisema mwili wa kichanga huyo uliopolewa na wananchi kutoka chooni humo na upelelezi wa kina wa kaya hadi kaya unaendelea ili kubaini mtuhumiwa huyo

No comments:

Post a Comment