KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 1, 2010

Namba za simu zisizosajiliwa kufungwa


MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema wananchi ambao hawajasajili namba zao hadi kufikia leo saa 6 usiku namba hizo zitafungiwa kupiga, kupokea simu pamoja na kutoa na kupokea ujumbe wa maandishi .
Mkurugenzi Mkuu waTCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo jana wakat akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa baada ya saa sita usiku ya leo Juni 30 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa itafungwa.

Alisema namba hiyo itafungwa kwa siku 90 na ifafunguliwa tena Septemba 30 mwaka huu.

Na namba hizo ifikapo Septemba 30 kma hazijasajiliwa tenea zitafutwa kwenye mitandao.

Kwa upande wa viongozi wa kampuni hizo za simu za mkononi walionekana kulalamikia hatua hiyo kwa kudai hatua hiyo itaweza kuwapotezea wateja na kuingia hasara kwa makampuni kwa kuwa zoezi hilo limeonekana kuwa gumu..

Walisema wangeomba muda uongezwe kwa kwua wateja wengi bado wameonekana hawajasajili laini zao na kuongeza kuwa muda uliotolewa hautoshi kukusanya data kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na wateja wengi kujitokeza nyakati za mwisho wa usajili huo

Nao watumiaji wa simu za mkononi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji walioenekana kulalalimia zoezi hilo kuwa gumu kwa kuwa kuna baadhi ya makampuni wakiulizia kama wameshasajiliwa hawapati majibu kwa muda muafaka.

NIFAHAMISHE ilishuhudia misururu ya foleni kila pembe ya jiji wakisubiri kusajiliwa na wengine wakionekana kurudia kusajili kwa kuwa waulizapo kwa namba husika ya *106# huambiwa bado hawajasajiliwa na huku wakidai walishasajili namba hizo.

No comments:

Post a Comment