KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 1, 2010

Achinjwa Kwa Shoka Kwa Kutembea na Mpenzi wa Mtu


MKAZI wa Uru Kusini mkoani Kilimanaro, aliyetambulika kwa jina la JAMES Kiwale (28), ameuawa kikatili baada ya kupigwa na shoka ya kichwa kwa kilichodaiwa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mchumba wa mtu.
James alikutwa na mkasa wakati alipokuwa akitoka makaburini kwenye mazishi ya jirani yake.

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Bw.Lucas Ng'oboko, amesema kuwa marehemu alipigwa na shoka kichwani na kupelekea kutenganishwa kati ya mwili na kichwa na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Joachim.

Alisema kijana huyo huyo aliamua kumpiga shoka mwenzake baada ya kumshuku kuwa alikiwa akitembea na mchumba wake aitwae Maria kitendo ambacho yeye hakukiafiki na kuchukua maamuzi hayo.

Aliendelea kusema kuwa ilidaiwa kuwa, marehemu wakati wa uhai wake alikuwa akitamba kuwa atahakikisha kuwa anatembea na mwanamke huyo jambo lililomsababishia hasira kali mtuhumiwa na kufanya kitendo hicho cha unyama.

Alisema mtuhumiwa huyo alimwekea mtego marehemu wakati anatoka kumzika jirani yake na kufanikiwa kumpiga shoka ya kichwa na kupelekea kichwa hicho kugawanyika mara mbili.

Alisema mara baada ya kufanya kitendo hicho mtuhumia huyo alikimbia na juhudi za jeshi hilo zinaendelea kumsaka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake

No comments:

Post a Comment