KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, July 13, 2010

Hispania ndio washindi mwaka 2010

Hispania imejinyakulia kombe la dunia katika mechi ya mwisho iliyochezwa jana usiku nchini Afrika kusini. Hispania iliwacharaza Uholanzi bao 1-0 katika dakika za ziada kutokana na bao la Andres Iniesta na hivyo kulipatia taifa hilo ushindi wake wa kwanza kabisa katika kombe hilo.

Uholanzi wamefikia fainali za kombe hilo mara tatu sasa bila mafanikio yoyote. Mechi hiyo iliyosisimua sana iliwapatia wachezaji wengi kadi ya manjano kwa kucheza rafu na hata mchezaji wa Uholanzi John Heitinger alirushwa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Hispania.



Dimba hilo la kombe la dunia lilimalizika kwa sherehe kuu ambapo Nelson Mandela mwenyewe alijitokeza kuwasalimia mashabiki waliohudhuria katika uwanja wa soka City mjini Soweto.

Mwandishi wa BBC amesema kinyang'anyiro hicho "kimekuwa mgeni njoo mwenyeji apone", maanake Afrika Kusini imepata ujenzi wa kifahari wa miji yake ya kuinua hadhi ya Afrika kwa jumla.

No comments:

Post a Comment