KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 1, 2010

Amuua Mfungwa Mwenzake na Kuyakaanga Mapafu Yake


Mfungwa mmoja nchini Ufaransa alimuua mfungwa mwenzake aliyekuwa akiishi naye chumba kimoja ili aweze kula moyo wake lakini kwa kutojua moyo una umbo gani aliishia kunyofoa mapafu ya mwenzake na kuyageuza mlo wa mchana.
Nicolas Cocaign, 39, mfungwa katika jela moja nchini Ufaransa anakabiliwa na kesi ya mauaji baada ya kumuua mfungwa mwenzake Thierry Baudry, 41, aliyekuwa akiishi naye chumba kimoja ili aweze kula moyo wake.

Lakini baada ya kukipasua kifua cha Baudry kwa mkasi alinyofoa mapafu yake akidhani ndio moyo.

Nicolas alitumia jiko la siri alilolitingeneza ndani ya chumba chake cha jela kuyaanga mapafu hayo kwa vitunguu na kujipatia mlo wake wa mchana.

Nicolas alipandishwa kizimbani jumatatu kujibu tuhuma za mauaji hayo yaliyoitingisha Ufaransa.

Inasemekana kuwa siku ya tukio Nicolas aligombana na Baudry ambaye walikuwa wakiishi chumba kimoja. Nicolas alitumia mfuko wa rambo kumbana pumzi Baudry mpaka alipohakikisha amefariki na kisha alitumia mkasi kukipasua kifua chake na kukiacha wazi.

"Nilikuwa na hamu ya kujua alikuwa na ladha gani", Nicolas aliwaambia wapelelezi wa kesi yake.

Nicolas alimvunja mbavu Baudry na kuchukua mapafu yake akidhani ndio moyo. Alikula sehemu ya mapafu hayo kama yalivyo na sehemu iliyobaki aliikanga kwa vitunguu.

Mfungwa mwengine, David Lagrue, alishuhudia tukio hilo na kutokana na kutishika sana kutokana na mauaji hayo, alijiua mwenyewe mwezi novemba mwaka jana.

Mwanasheria anayemtetea Nicolas, Fabien Picchiottino, aliiambia mahakama kuwa Nicolas ana matatizo ya akili na alitakiwa kuwekwa kwenye hospitali ya wagonjwa wa akili badala ya kufungwa jela.

"Mamlaka ya jela inabidi ibebe lawama kwa kushindwa kugundua kuwa Nicolas ana matatizo ya akili", alisema mwanasheria huyo.

Hukumu ya kesi hiyo itatolewa alhamisi.

No comments:

Post a Comment