KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 8, 2010

Ajiua Baada ya Brazil Kufungwa na Kutolewa Kombe la Dunia


Kipigo cha Brazil jana toka kwa Uholanzi kimepelekea kijana mmoja nchini Haiti ajiue mwenyewe kwa kujigongesha kwenye gari lililokuwa spidi.
Kijana mmoja nchini Haiti kutokana na huzuni za Brazil kufungwa na Uholanzi na kutupwa nje ya kombe la dunia, amejiua mwenyewe kwa kujigongesha kwenye gari.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 alifariki hapo hapo kwenye eneo la tukio katika kitongoji cha Nerette kilichopo nje kidogo ya mji mkuu wa Haiti.

Brazil ilitandikwa na Uholanzi mabao 2-1 kwenye mechi ya robo fainali na kutupwa nje ya kombe la dunia.

Nchini Haiti, Brazil ina washabiki wengi na Brazil ilipokuwa ikishinda mechi zake za kombe la dunia, watu walikuwa wakimiminika mitaani kushangilia.

Hali ilikuwa tofauti kidogo jana kutokana na kipigo hicho cha Brazil ambacho kimekiweka kibarua cha kocha wa Brazil, Dunga matatani.

No comments:

Post a Comment