KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, July 30, 2010

140 Wafariki Baada ya Boti Kupinduka nchini Kongo


Watu wapatao 140 wamefariki baada ya boti ya abiria iliyokuwa imejaza watu na mizigo kuliko uwezo wake kupinduka na kuzama kwenye mto uliopo nchini Jamhuri ya Kongo.
Ajali hiyo ilitokea kwenye mto Kasai uliopo katika mji wa Bandundu uliopo magharibi mwa Jamhuri ya Kongo.

Boti iliyopata ajali inasemekana ilikuwa imejaza watu wengi sana kuliko uwezo wake pamoja na mizigo mingi sana.

Boti hiyo ilikuwa ikisafiri kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Kinshasa wakati ilipopinduka na kuua watu waliokuwemo.

Wizara ya habari ya Kongo, imethibitisha vifo vya watu 80 kati ya watu 140 ambao wanahofia kupoteza maisha ndani ya boti hiyo.

Hili si tukio la kwanza kutokea katika mji wa Bandundu, mwezi novemba mwaka jana, boti nyingine ya abiria ilizama kwenye ziwa Mai-Ndombe lilipo kwenye mji huo na kupelekea watu 73 kupoteza maisha yao.

No comments:

Post a Comment