KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 24, 2010

Waziri mkuu mwanamke wa kwanza Australia


Julia Gillard ameapishwa kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke baada ya kufanyika kura ya uongozi wa chama cha Labor isiyotegemewa iliyomtoa Kevin Rudd.

Bw Rudd aliamua kutoshiriki kwenye kinyang'anyiro hicho akijua wazi atapata aibu baada ya kushindwa na naibu wake.

Bi Gillard amesema anaamini "serikali nzuri ilikuwa inapoteza mwelekeo" na alikuwa na nia ya kuifufua Labor kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa Oktoba.

Chama hicho kimepunguza wafuasi wake kwa kiasi kikubwa katika kura za maoni za mwaka huu.

Kubadilisha msimamo juu ya mfumo wa kaboni na ugomvi juu ya kodi ya migodi yenye utata zilisababisha imani za wengi kuhusu serikali ya Bw Rudd kushuka.

Bi Gillard, ambaye alikuwa naibu waziri mkuu kabla ya kupigwa kura hiyo siku ya Jumatano, aligombea bila kupingwa katika kura ya wabunge 112 wa chama cha Labor kwenye mkutano uliofanyika Alhamis asubuhi.

Waziri wa fedha Wayne Swan amechaguliwa kuwa naibu mpya, naye pia hakupingwa na yeyote.
Julia Gillard

Bi Gillard mwenye umri wa miaka 48 alizaliwa katika kisiwa cha Barry kusini mwa Wales, na kuhamia Australia na familia yake alipokuwa na umri wa miaka minne.

Alitiwa moyo kuwania uwaziri mkuu kutokana na wasiwasi kuwa chama cha Labour huenda kikashindwa katika uchaguzi mkuu ujao.

Mtangulizi wake, Kevin Rudd, alianza mwaka huu kama kiongozi aliyependwa zaidi na raia wa Australia kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita, lakini umaarufu wake uliporomoka alipoamua kuahirisha mpango wake wa kuyalinda mazingira, yaani kupunguza kiwango cha hewa chafu inayoruhusiwa kwenye anga zake.

Katika taifa ambalo raia wake wengi wanafurahia kukabiliana na maswala magumu, wengi waliona hatua hiyo kama ishara ya uoga.

Bw Rudd alilia hadharani mbele ya waandishi wa habari alipoona umashuhuri wake umeanguka

No comments:

Post a Comment