KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 26, 2010

Utata alipo Agathon wa Burundi


Waziri wa ulinzi wa Burundi amesema anatumai kiongozi wa chama kikuu cha upinzani na aliyekuwa kiongozi wa waasi Agathon Rwasa hajajificha.

Kauli hiyo ameitoa kufuatia ripoti kuwa Bw Rwasa, aliyetia saini makubaliano ya amani mwaka jana kusalimisha silaha, hajaonekana tangu Jumatano asubuhi.

Mapema mwezi huu alijitoa kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Jumatatu.

Uchaguzi huo utakuwa wa pili tangu kumalizika kwa mauaji ya kikatili ya wenyewe kwa wenyewe yaliyokuwa kwenye misingi ya kikabila yaliyodumu miaka 12.

Rais Pierre Nkurunziza na Bw Rwasa waliongoza zaidi kundi la waasi la Kihutu waliokuwa wakipigana dhidi ya jeshi la serikali lililodhibitiwa na Watutsi walio wachache.

Bw Rwasa alikataa kuacha mapigano wakati makundi mengine yalipoamua kuunda serikali ya muungano yaliyofuatiwa na uchaguzi mwaka 2005.

Aliiongoza National Liberation Force (FNL) kusalimisha silaha Aprili 2009 na amekuwa akidhaniwa kuwa mpinzani mkuu wa Rais Nkurunziza katika uchaguzi wa wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment