KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 26, 2010

WATU watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa kikatili


WATU watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali wakati watu hao wakiwa katika maandalizi kwenda kufanya uhalifu huko katika eneo la Mlowo wilayani Mbozi, mkoa wa Mbeya.
WAtu hao walidaiwa kabla ya kwenda kufanya tukio hilo walionekana majira ya asubuhi wakiwa katika baa moja maarufu iitwayo Furaha wilayani humo, wakinywa pombe wakati wakivuta muda wa kwenda kufanya uporaji waliopanga.

Ilidaiwa kuwa watu waliwahisi watu hao na kutoa taarifa polisi ambao walipofika mahali hapo majambazi hayo waliwatishia polisi kwa kutoa silaha zao hata hivyo hawakufanikiwa na walinyang’anywa silaha hizo.

Katika hali ya pulukushani kati yao polisi walionekana kuzidiwa nguvu na wananchi wenye hasira kali walichukua uamuzi wa kuwawasha moto watuhumiwa hao kwa kuwa walishakuwa wamefungwa pingu mikononi.

Watuhumiwa hao waliuawa kwa kumwagiwa mafuta aina ya petrol na kuwashwa moto na kuanza kuteketea kwa moto mbele ya polisi

No comments:

Post a Comment