KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, June 24, 2010

Vitu 10 kuhusu vuvuzela


Vuvuzela imekuwa nembo isiyo rasmi ya Kombe la Dunia mwaka 2010, na inaonekana kupendwa na kuchukiwa kwa kiwango sawa. Ifuatayo ni vitu 10 ambavyo huenda ukawa hujui kuhusu chombo cha pembe hiyo isiyo na ulinganifu wa sauti.
Vuvuzela ni nini hasa?

Ni pembe ya plastiki, yenye rangi ang'avu, na kuonekana kwa wingi katika matukio ya michezo Afrika Kusini. Vuvuzela za mwanzo zilizoonekana katika matukio ya michezo kwenye miaka ya mwanzo ya 90 yalitengenezwa kwa bamba za metali. Vuvuzela ya kawaida ina urefu wa sentimeta 65 lakini nyingine huweza kuwa hadi mita moja.
Asili yake ni wapi?

Hakuna anayejua. Hata hivyo imani kubwa iliyoenea ni kwamba ina uhusiano na pembe ya kudu iliyokuwa ikipulizwa kuwaita wanakijiji katika mikutano barani Afrika.

Hata hivyo, mapema mwaka huu, kanisa la ubatizo la Nazareth limedai kuwa vuvuzela ni yao, inayotumiwa na waumini wake kwenye hijja, na kutishia kuchukua hatua za kisheria kuzuia zisitumiwe kwenye Kombe la Dunia.
"Vuvuzela" ina maana gani?

Inaoenakana bado ni suala linalojadilika. Wengine wanadhani imetoka kwenye lugha ya Kizulu ikimaanisha "kupiga kelele." Wengine wanasema ni lugha ya mtaani ikimaanisha "nyunyiza" kwasababu "inawanyunyizia watu muziki". Wengi wanaamini inamaanisha "vuta".
Ilikuwaje mpaka ikaishia kutumika kwenye viwanja vya mpira?

Kanisa la Kibabtisti la Nazarath limesema "lilipoteza" vuvuzela katika miaka ya 90 wakati mfuasi wa timu kubwa ya mpira ya Afrika Kusini alipotembelea kanisa hilo. Aliposhindwa kuchukua chombo hicho kirefu cha metali ndani ya viwanja vya mpira, akaiunda upya kwa plastiki.

Wanaotengeneza vuvuzela wamesema walianza kutengeneza chombo hicho kwa wingi baada ya asili ya chombo hicho kwa kutumia bati ilipoanza kuonekana kwenye michezo miaka ya 90.
Sasa elezea sauti?

Mlio halisi wa vuvuzela unasemekana kuwa ni nzito.

Ikipulizwa yenyewe, hufananishwa na sauti ya ushuzi wa tembo. Kukiwa na mechi ya mpira iliyojaa mashabiki wanaopuliza chombo hicho, sauti hiyo husikika kama bumba la nyuki wenye hasira.
Huenda ikawa inakera, lakini ina madhara?

Utafiti uliofanywa hivi karibuni umegundua kuwa kiwango cha sauti kinachotoka kwenye vuvuzela, kwa nguvu zote na inapokandamizwa kwenye sikio lako, hufikia kizio cha kupimia kiwango cha sauti 127.

Hii ni sauti kubwa zaidi ya ngoma ikiwa katika kizio cha kupimia kiwango cha sauti 122, msumeno wa mnyororo katika kizio cha 100 na mluzi wa refa kwa kizio cha 121.8.

Wakfu wa Hear the World, iliyoundwa na shirika la kutengeneza vifaa vya kusikia la Uswizi, Phonax inayoelimisha watu kuhusu kupoteza uwezo wa kusikia, imeonya kuwepo eneo la makelele mengi kwa muda mrefu kunahatarisha uwezekano wa kutosikia kabisa.

Wamekuwa wakiwasihi mashabiki kujilinda kwa kutumia vizibo vya masikio.

Baadhi ya wamiliki wa duka Afrika Kusini wamesema wameishiwa na vizibo hivyo vya masikio viitwavyo Vuvu-Stops.
Kuna athari nyingine za kiafya??

Daktari mmoja wa Uingereza ameonya kwamba vuvuzela inaweza pia kueneza mafua na vijidudu vya mafua.

Dr Ruth McNerney, wa London School of Hygiene na Tropical Medicine, amesema chombo hicho kina uwezo wa kumwambukiza maradhi yule aliyekaa karibu na anayepuliza vuvuzela hiyo kwasababu "pumzi nyingi hupita kwenye chombo hicho."

Amesema utafiti wa hivi karibuni umegundua kwamba kipulizo hicho, vitonye vidogo vinavyoweza kubeba vijidudu vya mafua, vimeonekana sehemu ya chini ya vuvuzela baada ya watu kuzipuliza.

Dr McNerney amesema vitonye hivyo ni vidogo kiasi cha kuweza kukaa hewani kwa saa kadhaa, na huweza kupenya kwenye njia ya upepo ya mapafu ya mtu.
Kwa hiyo watu wanasemaje kuhusu vuvuzela???

Wachezaji wengi walilalamika kuhusu vuvuzela ziliposikika kwa mara ya kwanza kwenye kombe la shirikisho mwaka jana.

Kocha wa Uholanzi Bert van Marwijk amezizuia kutumika kwenye mazoezi ya timu zao, na Cristiano Ronaldo wa Ureno alikiri wiki hii: "Ni vigumu sana kwa mtu yeyote kucheza uzuri."

Hata mashabiki wengine wanaotazama mechi hizo kupitia televisheni wameripoti kuwa inabidi watoe sauti kukwepa sauti hiyo kali.
Bila shaka watu wengine mbali na Waafrika Kusini lazima watakuwa wanazipenda

Ndio. Zimepitishwa kwa moyo mmoja na Rais wa Fifa Sepp Blatter ambaye amesema hatozipiga marufuku.

Amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, "Afrika ina mahadhi tofauti, sauti tofauti" na ni utamaduni muhimu miongoni mwa mashabiki wa Afrika Kusini inayostahili kufurahiwa.

Mchezaji wa England Jamie Carragher amesema atachukua baadhi ya vuvuzela akirudi nyumbani. "Nimekuwa nikizungumza na wanangu kwa simu na wanataka vuvuzela mbili. Ninazo mbili kwenye mkoba wangu tayari."
Je utata huu umeathiri mauzo?

Neil van Schalkwyk amesema kampuni yake imeuza vuvuzela milioni 1.5 barani Ulaya tangu mwezi Oktoba na anatarajia mauzo kufikia milioni 20 katika kipindi cha mashindano ya Kombe la Dunia.

Brandon Bernardo wa wavuti ya vuvuzela.co.za ameiambia shirika la habari la Reuters wanaweza kuuza takriban vuvuzela 10,000 kwa siku.

Amesema, " Tumeziuza zote."

Hata bila ya Kombe la Dunia, biashara ya vuvuzela na Afrika Kusini inasadikiwa kuwa na thamani ya takriban dola za kimarekani milioni 6.45.

No comments:

Post a Comment