KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, June 8, 2010
UN kuwekea Iran vikwazo vipya
Baraza la usalama la umoja wa matiafa limeafikia azimio la kuiwekea Iran vikwazo vipya na linatarajiwa kupigia kura azimio hilo hapo kesho.
Vikwazo hivyo vinalenga kudhibiti miradi ya Nuclear ya Iran, na iwapo vitaidhinishwa basi vitaongeza ukaguzi wa bidhaa zinazoingizwa nchini humo na kupunguza kuuziwa nchi hiyo silaha.
Mwandishi wa BBC katika umoja huo amesema kuwa kuna baadhi ya nchi ambazo hazitarajiwi kupigia kura azimio hilo japo hazina kura ya turufu.
Waziri mkuu wa Iran Mahamoud Ahmedinajad
Uturuki na Brazil wamesisitiza kuwa vikwazo vipya kwa Iran vitahujumu uhusiano mwema katika eneo hilo na wamesema kuwa kuna matumaini ya kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia kutokana na makubaliano ya kubadilishana mafuta ya nuclear walioafikia hivi majuzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment