MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema amelaani kitendo kilichofanywa na wakazi wa Hedaru na kutaka kufunga vituo vya polisi ambavyo havina silaha.
Mwema amesema kwua jeshi hilo hlitavumilia uharibifu huo na kuwachukuliwa hatua kali wote watakabainika kuhusika na matukio hayo ya uvunjaji wa sheria.
IGP Mwema alisema kuwa, nchi haiwezi kuendeshwa kwa fujo na kuwa vitendo hivyo vinarudisha nyuma juhudi za jeshi hilo na kulipa hasara.
Alisema kuwa wananchi wanaharibu miundombinu ya jeshi hilo, na wananchi kuendelea kuamini imani potofu na kusababisha matukio ya kuchomana moto wenyewe kwa wenyewe na sasa wamehamia kwenye vituo vya polisi jambo ambalo halitafumbiwa macho.
Alisema wananchi hao hawakuwa na sababu ya kucoma moto kituo kwa sababau watu hao waliokolewa na polisi na hakuwa na uhakika kama ni kweli mtoto aliuawa ama la, na endapo mtoto akipatikana yuko hai wangelieleza nini jeshi la polisi
“Hatutawavumila wale wote waliohusika ktika tukio hilo” alisema I|GP
No comments:
Post a Comment