KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

Maharamia Wakisomali kushtakiwa Ujerumani

Washukuwa kumi wa uharamia raia wa Somalia wanatarajiwa kuhamishwa kutoka Uholanzi na kufikishwa mahakamani nchini Ujerumani.

Mahakama moja mjini Amsterdam iliidhinisha washukiwa hao kuhamishiwa Ujerumani baada kukataa madai ya upande wa utetezi ya kutaka washtakiwe nchini Uholanzi.

Washukiwa hao kumi walikamatwa kikosi maalum cha wanamaji wa Uholanzi baada ya kushambulia meli ya mizigo ya Ujerumani nje ya pwani ya Somalia mwezi April.

Waendesha mashtaka mjini Hamburg nchini Ujerumani wanatarajiwa kuwashtaki washukiwa hao kwa kosa la utekaji nyara.



Jaji katika mahakama ya Amsterdam aliamua kuwa licha ya Uholanzi kuwa na mamlaka ya kuwashtaki washukiwa, hakuna sababu za kutosha za kukataa kuwapeleka Ujerumani kushtakiwa.

Mawakili wa utetezi wamedai kuwa meli iliyoshambuliwa ilikuwa na usajili wa Bahamas na wala si Ujerumani akama ilivyodaiwa.

"Ikiwa tunaweza kuhakikisha kuwa hatujui meli hiyo ilikuwa na bendera ya nchi gani, ikiwa tuna uhakika kuwa hakuna nyaraka, nani mmiliki wa meli, kwa nini mahakama inasema hivyo kiurahisi, inatosha, kuwa mnapaswa kwende Ujerumani?" wakili Michael Balemans aliliambia shirika la habari la Reuters.

Meli ya MV Taipan ilitekwa nyara kiasi cha km 900 mashariki kwa pwani ya Somalia mapema mwezi April.

Manuari ya Uholanzi, iliyokuwa ikishika doria kwenye maji ya Somalia ikiwa sehemu ya Muungano wa Ulaya ya kupambana na uharamia, ilillazimika kuchukua hatua baada ya kupokea ishara ya hali ya dharura.

No comments:

Post a Comment