KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, June 2, 2010

Mahakamani Kwa Kumlawiti Mtoto wa Miaka Minane

KIJANA mmoja jina linahifadhiwa kwa sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka minane.
Kijana huyo mkazi wa Manzese Darajani jijini Dar es Salaam amedaiwa kufanya kosa hilo Mei 29, mwaka huu, majira ya mchana huko maeneo ya Magomeni Kagera jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa kijana huyo alifika nyumbani kwa kaka yake maeneo ya Magomeni Kagera kwa lengo la kumtembelea lakini alipoondoka ndipo wazazi wa mtoto huyo wa kiume walipogundua uharibifu aliofanya.

Imedaiwa kuwa mara baada ya kijana huyo kuondoka, mtoto huyo alionekana kuwa tofauti na amekuwa kama mnyonge na alishindwa hata kutembea sawasawa na alipoulizwa alisema alikuwa na kijana huyo chumbani.

Na alipofanyiwa uchunguzi aligundulika kufayiwa tendo hilo na ndipo taarifa zikafikishwa kituoni mara moja na kijana huyo alitiwa mbaroni na kufikishwa kituoni kwa maelezo ya kina.

Hata hivyo kijana huyo alikana kuhusika na tukio hilo na taratibu za kipolisi zinafuatwa na zitakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka hayo.

No comments:

Post a Comment