KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, June 2, 2010

Akimbilia Dar baada ya kumkung’uta mke mwenzake

MWANAMKE Fatma Said [26]mkazi wa Tungi Morogoro, amejikuta akikimbilia jijini Dar es Salaam baada ya kumpa kichapo cha nguvu mke mwenzake baada ya kumvurugia utaratibu wa ndoa waliopeana wawili hao na kukimbilia huko kwa kujificha.
Mwanamke huyo amejikuta amefika jijini Dar e s Salaam na kufikia kwa dada yake maen.

MWanamke huyo alimueleza dada yake amekuja kupumzika kwa muda na ataondoka baada ya wiki mbili.

Dada yake alitia shaka maelezo hayo kwakuwa alijua mdogo wake ni mwanandoa. Kabla ya kumkubalia dada yake huyo alimuuliza kama mume wake alikuwa anafahamu ujio wake huyo na kama alikuwa amemruhusu.

Alimwambia aliruhusiwa na alielewa safari hiyo ya kuja kupumzika huko.

Dada yake huyo alikuwa na wasiwasi na majibu hayo na aliamua kufanya mawasiliano na mama yao anayeishi karibu na mdogo wake huyo.

Mama yake alishangazwa na habari ya binti yake kufika jijini Dar es Salaam kwa kuwa mume wake alifika juzi kwake kumuuliza mkewe yupo kwake.

Kutokana na majibu ya mama yake, dada huyo aliamua kufanya mawasiliano na shemeji yake mume wa dada huyo na kumtega kwa kumuuliza hali zao huko yeye na mke wake wanaendeleaje?’ na kujibiwa kuwa hajui mkewe ameenda wapi kwa kuwa ni siku mbili zimepita hajui alipo.

Baada ya kupata majibu hayo alimtaka mdogo wake afunge virago vyake arudi kwa mumewe na ndipo alipoanza kumueleza dada yake huyo alikimbilia huko kwa kuwa alipigana na mke mwenzake na kumjeruhi vibaya.

Alijieleza kuwa alikasirishwa na kitendo na mke mwenzake huyo ambaye ni mke mkubwa kwa mume wao kuvuruga utaratibu waliojiwekea wa zamu za kuishi na mume huyo.

Alidai kuwa yeye na mke mwenzake huyo walikubaliana kuwa na zamu ya siku tatu lakini mwenzake alizidisha na kukaa nae siku tano na ndipo alipoamua kwenda nyumbani kwake kufanya fujo na kumjeruhi vibaya mke mwenzake huyo.

“Ndio mana nimekuja huku dada nipumzike kidogo wala sijamuaga mume wangu".

Hata hivyo dada yake hakukubaliana na maelezo yake na alisisitiza achukue virago vyake arudi kwa mumewe.

No comments:

Post a Comment