KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 10, 2010

Cole na Ballack kuihama Chelsea


Klabu ya Chelsea ya Uingereza imethibitisha kwamba wachezaji Joe Cole na Michael Ballack watakihama klabu wakati wa msimu huu wa joto kabla ligi kuu ya Premier ya England kuanza.


Ballack na Cole kuihama Chelsea
Wachezaji hao watajiunga na vilabu vingine chini ya mpango wa kubadilishana wachezaji.

Cole, mwenye umri wa miaka 28, ataondoka mwanzoni mwa mwezi Julai.

Mchezaji huyo anachukua hatua hiyo baada ya mabingwa wa ligi kuu ya Premier ya England, kutangaza kwamba hawatamuongezea muda zaidi kukichezea klabu.

Mchezaji huyo wa kiungo cha kati alijiunga na Chelsea kutoka West Ham mwaka 2003.

Wakati huo alinunuliwa kwa pauni milioni 6.6.

Hivi sasa yuko nchini Afrika Kusini kucheza katika michuano ya Kombe la Dunia.

Mjerumani kiungo cha kati, Ballack, na mwenye umri wa miaka 33, naye amekuwa na Chelsea tangu mwaka 2006.

Yeye pia hataongezewa muda katika mkataba wake kuichezea Chelsea.

Ballack alitazamiwa kukiongoza kikosi cha Ujerumani kama nahodha katika mashindano ya Kombe la Dunia, lakini aliumia katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya timu ya Portsmouth, na kutangazwa kama hataweza kuichezea nchi yake.

Mkataba wake utakwisha mwisho wa mwezi huu wa Juni.

Ballack alisajiliwa na meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho, kwa kumchukua pasipo malipo kutoka kwa klabu ya Bayern Muniich ya Ujerumani, mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment