KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 5, 2010

Cole huenda akahama Chelsea- Redknapp

Meneja wa klabu ya Tottenham, Harry Redknapp amesema yuko tayari kumsaini mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Joe Cole ambaye amemaliza mkataba wake wa klabu hiyo.

Redknapp alikuwa meneja wa mchezaji huyo wakati alipokuwa akiichezea klabu ya West Ham na angelipenda kukutana tena na mchezaji huyo wa uingereza msimu ujao.

Cole mwenye umri wa miaka 28, ameshindwa kujihakikishia nafasi katika kikosi cha wachezaji 11 wa kwanza wa Chelsea huku kandarasi yake ikielekea kumalizika baadaye mwaka huu.

Redknapp aliyasema hayo kufuatia kujumuishwa kwa Cole kwenye kikosi cha Uingereza, kitakachoshiriki kwenye dimba la dunia baadaye mwezi huu nchini Afrika Kusini, chini ya meneja Fabio Capello.

Kocha huyo amesema ikiwa Chelsea haitahitaji huduma za mchezaji huyo, basi klabu iyakayofanikiwa kumsajili itakua imejinyakulia mchezaji wa kutegemewa.

No comments:

Post a Comment