KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, June 21, 2010

Australia yaikatalia Ghana, 1-1
Ghana ilitoka sare 1-1 na Australia katika mechi ya Kundi D kwenye uwanja wa Royal Bafokeng mjini Rustenburg, licha ya Australia kuwa na wachezaji 10 baada ya Harry Kewell kuonyeshwa kadi nyekundu.

Matokeo hayo yameiweka Ghana katika hali tete ya kufuzu raundi ya pili ya Kombe la Dunia, ikisubiri mechi yake ya mwisho ya makundi dhidi ya Ujerumani, Jumatano ijayo.

Ujerumani ilishindwa na Serbia bao 1-0 siku ya Ijumaa, na njia pekee kwa timu hiyo kufuzu raundi ya pili ni kuishinda Ghana.

Ikiwa Ujerumani itaishinda Ghana siku ya Jumatano, nayo Serbia ipate ushindi dhidi ya Australia, basi Ghana itakuwa imeyaaga mashindano.

Kadi nyekundu
Harry Kewell alionyeshwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 25 baada ya kuzuia kwa mkono shuti la Jonathan Mensah karibu na lango la Australia.

Pamoja na Kewell kuonyeshwa kadi nyekundu, refa kutoka Italia, Roberto Rossetti aliwapa Ghana penalti , ambayo Asmaoah Gyan alifunga.

Lilikuwa bao la kusawazisha baada ya Australia kutangulia kufunga katika dakika ya 11 kupitia mshambuliaji Brett Holman.

Katika mechi ya ufunguzi Australia ilikuwa imefungwa na Ujerumani 4-0.

Ghana walifanya mashambulizi ya mara kwa mara lakini umaliziaji wao ukawa mbaya.

This content requires Flash Player version 10 (installed version: No Flash Flayer installed, or version is pre 6.0.0

No comments:

Post a Comment