KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 3, 2010

Watu waliokuwa wamejihami kwa mapanga wamemuua mwanamke Albino na mtoto wake


Watu waliokuwa wamejihami kwa mapanga wamemuua mwanamke Albino na mtoto wake wa miaka minne nchini Burundi.

Inaarifiwa kuwa maiti za wawili hao ilikatwakatwa vibaya katika mkoa wa Cankuzo, unaopakana na Tanzania.

Mwenyekiti wa chama cha maalbino nchini humo, Kassim Kazungu, ameelezea BBC kuwa anashuku wauaji walitoroka gerezani na walikuwa wamehukumiwa kwa makosa ya kuwashambulia maalbino.

Aliongeza kuwa shambulio kama hilo halijashuhudiwa Burundi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa viungo vya mwili wa albino vinaweza kuwatajirisha.

No comments:

Post a Comment