KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 3, 2010


Haramia wa kisomali karibu na mji wa Hobyo


Maharamia wanaoshikilia meli katika mji wa Harardhere nchini Somalia wamelazimika kuhamisha meli hizo baada ya wapiganaji wa kiislamu kuuteka mji huo.

Msemaji wa maharamia hao Ali Omar amesema meli hizo zilizobeba wahudumu sitini zimepelekwa katika eneo la Hobyo,karibu kilomita mia moja kaskazini mwa Harardhere. Mwishoni mwa juma kundi la Hizbul Islam liliutwaa mji huo


Mvuvi katika eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ulikuwa na meli tatu karibu na pwani ya Harardhere lakini leo asubuhi hawakuziona.

Kundi hilo linasema linataka kukabiliana na visa vya uharamia lakini ripoti zaidi zinasema wapiganaji hao walitaka kuzungumza na maharamia hao ili waweze kujipatia sehemu ya fedha za kikombozi zinazotolewa ili kufanikisha kuachiliwa huru kwa meli hizo na wahaudumu wake.

Mwandishi wa BBC anasema makampuni ya meli yanafutilia kwa makini hatua itakayochukuliwa na wapiganaji wa Hizbul Islam ili kuona kama visa vya uharamia vitapungua au vitaongezeka.

Katika miaka ya hivi karibuni maharamia wameteka meli nyingi katika Bahari ya Hindi na kupelelea nchi kadhaa kutuma manuari za kivita kushika doria katika bahari hiyo.

Kulikuwa na meli tatu karibu na pwani ya Harardhere lakini asubuhi hii hatukuziona,zilipelekwa Hobyo nafikiri maharamia wanaogopa wapiganaji wa Hizbul Islam na ndio sababu wamekimbia

No comments:

Post a Comment