KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 13, 2010

Watoto wenye vichwa vikubwa watatibiwa bure


SERIKALI imetangaza kwamba watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na wale wenye matatizo ya uti wa mgongo watapata matibabu hayo nchini bure katika taasisi ya mifupa MOI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Blandina Nyoni ameyasema hayo wkati wa mkutano maalumu wa kuzungmza na wazazi wenye watoto wenye matatizo hayo jijini Dar es Salaam.

Serikali kupitia Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili, MOI, imeamua kuanza kutoa matibabu kwa watoto hao bure katika taasisi hiyo.

Amesema awali matibabu hayo yalikuwa yakitolewa na Hospitali za nje na CCBRT.
Amesema awali taasisi hiyo ilikuwea inatoa huduma hiyo lakini kutokana na matatizo ya kiufadhili ilisitisha huduma hiyo na sasa imerudisha huduma hiyo kutokana na wazazi wengi hawana uwezo wa kutibia watoto hao.

Amesema kwa upande wa Serikali imejidhatiti na itahakikisha hakuna mtoto yeyote anayekosa kupata matibabu kwa sababu mzazi wake hana uwezo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Prof. Lawrence Museru amesema Hospitali yake imeamua kuchukua jukumu hilo baada ya kuona matatizo hayo yanazidi kuwa makubwa na wazazi kujikuta hawana pa kuwapeleka kutokana na hospitali nyingi kutokuwa na uwezo wa kuwahudumia.

Prof. Museru ameeleza kuwa taasisi hiyo inatumia njia ya kisasa inayojulikana kama ETV kwa ajili ya kuwahudumia watoto hao.

No comments:

Post a Comment