KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 12, 2010

Waasi watishia vita upya Sudan

Moja ya kundi kuu la waasi katika eneo la Darfur nchini Sudan, limetishia kuanzisha "vita vikali" iwapo kiongozi wake atakamatwa.

Maafisa wa Sudan wamewataka polisi wa kimataifa, Interpol, kumkamata kiongozi wa kundi la Justine and Equality Movement (Jem) Khalil Ibrahim kwa kupanga mashambulio huko Omdurman mwaka 2008.
Mashambulizi Mapya

Jem ilitia saini makubaliano ya kusimamisha mapigano na serikali mwezi Februari, lakini kundi hilo liliondoka katika meza ya mazungumzo ya kutafuta amani mapema mwaka huu kwa kudai serikali imeanzisha mashambulizi mapya.


Kiongozi wa Jem Khalil Ibrahim
Bw Khalil anadhaniwa kuwepo nchini Misri. Misri ni mshirika wa Sudan.

Mwenyekiti wa masuala ya kisheria wa Jem, Eltahir Adam Elfaki ameiambia BBC kuwa "Jitihada zozote za kutaka kumkamata Dokta Khalil zitasababisha vika vikali."

"Hata tunavyozungumza, serikali ya Sudan inarusha mabomu Kaskazini na Magharibi mwa Darfur" amesema mwenyekiti huyo. Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) imetoa amri ya kukamatwa kwa rais Omar al-Bashir kutokana na tuhuma za uhalifu wa kivita uliofanywa huko Darfur. Bw Bashir anakanusha vikali madai hayo.

Jitihada zozote za kutaka kumkamata Dokta Khalil zitasababisha vika vikali
Eltahir Adam Elfaki

Baada ya Jem kutia saini, bw bashir alitangaza kuwa vita vya Darfur "vimekwisha".

Kundi jingine la waasi Darfur, Liberation and Justice Movement (LJM) pia lilitria saini kusitisha mapigano kabla ya uchaguzi.
Darfur Kimya

Hata hivyo kundi jingine kutoka ndani ya kundi la Sudan Liberation rmy (SLA) linaloongozwa na Abdul Wahid, bado anapambana na serikali na amekataa kushiriki katika mazungumzo ya kutafuta amani.

Darfur ilikuwa kimya wakati wa uchaguzi wa kihistoria mwezi Aprili, uchaguzi ulioshuhudia bw Bashir akichaguliwa tena kuwa rais.
Hata hivyo uchaguzi haukufanyika katika maeneo mengi ya Darfur kutokana na wasiwasi wa hali ya usalama.

Tangu mzozo wa darfur kuanza mwaka 2003, watu wapatao milioni mbili na nusu wamekimbia makazi yao, na Umoja wa mataifa unasema watu wengine laki tatu wamekufa kutokana na mzozo huo.

Serilai inasema takwimu hizo zimekuzwa, na inakanusha madai kuwa iliwaunga mkono wanamgambo wa Kiarabu kwa kuua makabila ya watu weusi.

No comments:

Post a Comment