KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, May 16, 2010

Thailand: Amri ya mwisho kwa waandamanaji

Serikali ya Thailand imetoa agizo la mwisho kwa waandamanaji walioweka kambi mjini Bangkok tangu mwezi Machi, ikiwataka wanawake na wazee kuondoka eneo hilo ifikapo Jumatatu mchana.

Shirika la Msalana Mwekundu limeombwa kuwashawishi watu kuondoka kwenye maandamano hayo, ambako watu wanataka Waziri Mkuu, Abhisit Vejjajiva, ajiuzulu.

Kiongozi wa mmoja wa waandamanaji alisema Thailand inakaribia kutumbukia katika "vita vya wenyewe kwa wenyewe" baada ya machafuko kusababisha vifo vya watu wasiopungua 25.


Maelfu wa wananchi wanaandamana katika sehemu nyingine ya mji huo.

Kiongozi wa maandamano hayo yajulikayo kama Red-shirt, Nattawut Saikua, alinukuliwa akisema waandamanaji wako tayari kushiriki katika mazungumzo yatakayosimamiwa na Umoja wa Mataifa kumaliza mvutano huo, lakini kwa masharti serikali iondoe majeshi yake mitaani.

Lakini sheika la habari la Reuters lilitaarifu kuwa serikali imekataa pendekezo hilo.

No comments:

Post a Comment