KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, May 21, 2010

Siku Mbili zaidi Za kujiandikisha Kupiga Kura

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi vituoni ili waweze kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
KESHO na keshokutwa ndiyo fursa nyingine kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao hawakupata muda wa kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa siku nyingine mbili ambazo ni Jumamosi Mei 22 na Jumapili Mei 23 kwa wasiojiandikisha wajiandikishe katika daftari la wapiga kura ili waweze kupiga kura katika uchanguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

"Tunaomba wajitokeze ili waweze kupiga kura na asiyejiandikisha hataweza kupiga kura" ilisisitizwa

Pia viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wametumia fursa hiyo kupita ktika kata mbalimbali kuwakumbusha wakazi wasiojiandikisha waende wakajiandikishe ili waweze kuchagua viongozi wawatakao katika uchaguzi ujao.

No comments:

Post a Comment