KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, May 11, 2010

Mjerumani Afunga Ndoa Na Paka


Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani amefunga ndoa na paka wake kipenzi baada ya madaktari wa wanyama kumwambia kuwa paka wake ambaye ni mgonjwa hana siku nyingi atafariki.
Gazeti la Bild la nchini Ujerumani limeripoti kwamba Uwe Mitzscherlich mwenye umri wa miaka 39 aliamua kufunga ndoa na paka wake baada ya kuambiwa kuwa paka wake huyo ambaye ni mgonjwa hana uhai mrefu.

Gazeti la Bild liliripoti kuwa Uwe alimlipa msanii euro 300 (Takribani Tsh. 540,000) ili aigize kama afisa wa kufungisha ndoa kwenye sherehe aliyoiandaa kwakuwa ni kinyume cha sheria kufunga ndoa na mnyama nchini Ujerumani.

Uwe alisema kuwa alitaka kufunga ndoa ya kweli na paka wake anayeitwa Cecilia kabla hajafariki kutokana na ugonjwa wa asthma.

Uwe ameishi na bi harusi wake ( paka wake) kwa zaidi ya miaka 10.

"Cecilia ni myama muaminifu, tunakumbatiana kila wakati na siku zote amekuwa akilala kwenye kitanda changu", alisema Uwe ambaye ni mfanyakazi wa posta katika mji wa Possendorf akiliambia gazeti la Bild.

Msanii Christin-Maria Lohri, ambaye ndiye aliyefungisha ndoa hiyo alisema "Mwanzoni nilifikiri ananitania lakini baadae niligundua kuwa Uwe alikuwa hatanii na hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake aliyokuwa akiisubiria iwe kweli".

No comments:

Post a Comment