KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Ligi mashuhuri za ulaya zafikia kilele


Bundesliga:Munich na schalke-premier League-Manu na Chelsea na La Liga:Barca na Real Madrid.

Ligi mashuhuri za ulaya, zinaingia kilele chake mwishoni mwa wiki hii kabla kumalizika kabisa mwishoni mwa wiki ijayo:Katika Bundesliga ,kinyan'ganyiro kileleni ni kati ya mabingwa mara kadhaa Bayern Munich na Schalke -zote zikiwa pointi sawa.Katika Premier League-ligi ya Uingereza , kinyan'ganyiro ni kati ya Chelsea na Manchester United na katika La Liga-ligi ya Spian,FC Barcelona,baada ya kuvuliwa juzi taji lao la ulaya la champions League na Inter Milan ya Itali , iko pointi 1 tu mbele ya mahasdimu wao Real Madrid.

Baada ya kukata tiketi yake ya finali ya champions league kati yake na Inter Milan hapo juzi, Bayern Munich ,imeondoa shaka shaka zote kwamba, msimu huu ina azma ya kutoroka na vikombe 3:Champions League hapo Mei 22,taji la Bundesliga na la Ujerumani (DFB Pokale).

Mahasimu wao Schalke, wamepania kuwatilia kitumbua chao mchanga alao katika Bundesliga,kwani, Munich na Schalke zote zina pointi sawa 64 isipokuwa Munich inaoongoza kwa magoli.

Munich inahitaji kwahivyo, kushinda leo dhidi ya Bochum iliopo mkiani mwa Lig na iliomtimua juzi kocha wake Heiko Herrlich na kumuachia usukani wa kuiongoza Bochum leo,stadi wa zamani Dariusz Wosz .Wosz anakuwa kocha 4 kwa bochum msimu huu .Bochum inajua lazima iishinde Munich leo kubakia hayi katika Bundesliga ama sivyo,itarudi daraja ya pili msimu ujao.

Schalke, ina kibarua kigumu zaidi na haimudu kushindwa ikiwa iweke hayi matumaini ya ubingwa.Inacheza na Werder Bremen ,lakini iko nyumbani.Inahitaji pointi zote 3 ili kuendeleza changamoto na Bayern Munich hadi Jumamosi ijayo ili kujua: nani msimu huu atavaa taji la bundesliga.

Bayer Leverkusen , iliongoza Bundesliga muda mrefu, imeteleza hadi nafasi ya 3 na ina miadi jioni hii na timu ya mkiani Hertha Berlin.Berlin, takriban imesharudi daraja ya pili.

FC Cologne, imeepuka msiba ulioipata Hertha Berlin,kwani imeshafuzu kusalia daraja ya kwanza na leo, ina miadi nyumbani na Freiburg.Mabingwa Wolfsburg, wanacheza na Borussia Dortmund,Frankfurt na Hoffenheim.Hamburg iliomtimua kocha wake Bruno Labbadia na kupigwa kumbo juzi nje ya finali ya Ligi ya Ulaya na Fulham ya Uingereza, inacheza na Nuremberg.Stuttgart, inakamilisha kalenda ya mwishoni mwa wiki hii kwa mpambano kesho na Mainz.

Katika Premier League,Chelsea na Manchester United ,kila moja imebakisha mapambano 2 kabla kujua nani ataibuka bingwa: Kesho Chelsea ina miadi na Liverpool na wiki ijayo na Wigan Athletic.Manchester inaipambana kesho na Sunderland kabla haikufunga msimu huu na Stoke City.Mshambulizi wa Manu, Wayne Rooney na beki-mshahara Rio Ferdinand,watazamiwa kuwa fit kuteremka kesho uwanjani .Wote wawili wakiugua. Rooney, ameshatia mabao 34 msimu huu.

Huko Spain, La Liga pia inanyemelea pia kilele chake :Mabingwa FC Barcelona, wanauguza majaraha waliopata katika Champions league kati ya wiki walipopigwa kumbo na Inter Milan. Wanatumai alao kufuta machozi kwa kutwaa ubingwa wa Spain. Kikosi hiki cha kocha Pep Guardiola,kinaongoza kwa pointi 1 kabla mpambano wa leo na Villarreal.Mahasimu wao Real Madrid, watakuwa kesho uwanjani wakicheza na Osasuna. Ikiwa Barca itavuliwa pia taji la Spain kama walivyovuliwa lile la Ulaya, ni swala la kusubiri kuona.Mashabiki wake lakini wanadai, watabakia wafalme wa dimba la Spain.

Mwandishi: Ramadhan Ali /DPAE/RTRE

Uhariri: S.Kitojo

No comments:

Post a Comment