KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Kwanini BP bado haijadhibiti kuvuja mafuta Ghuba la Mexico?


Je, mchango wa Mabenki kuiokoa Ugiriki ukaribishwe ?

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo yamechambua mada mbali mbali -usoni kabisa vipi kukifumbua kitandawili cha madeni ya Ugiriki na kuiokoa sarafu ya Euro isizidi kuteremka thamani ?:

Hata mripuko katika Jukwaa la kisima cha mafuta katika ghuba la Mexico na athari zake kwa mwambao wa pwani wa Marekani ni mada ambayo bado inazungumzwa.

Braunschweiger Zeitung juu ya kuvuja mafuta laandika:

"Bado mafuta ya petroli yanavuja mfululizo na kuchafua bahari.Wiki 2 tangu kuzuka mripuko katika Jukwaa la kuchimbia mafuta katika Ghuba la Mexico,kampuni la mafuta la BP, limeshindwa kudhibiti uchafuzi wa mazingira na dhara zake.

Kampuni la mafuta la BP, lilipaswa na mapema zaidi kuchukua hatua .....Lakini yabainika maarifa ya mabingwa wake hayatoshi.Hadi sasa kifuniko cha chuma cha kuziba bomba hilo linalovuja, kilifanyiwa majaribio katika maji ya kina cha chini .Tundu inayovuja mafuta lakini, iko kina cha chini sana cha hadi mita 1500.Swali: inakuaje : Kampuni kubwa la uchimbaji mafuta kama BP linaekeza mamilioni ya Euro katika uchimbaji mafuta,lakini halimudu kuwa na kufulu la chuma lenye uwezo wa kuziba tundu inayovuja mafuta ?"

Likitugeuzia mada ,ufumbuzi wa wa tatizo la madeni ya Ugiriki na athari zake kwa thamani ya Euro, uko wazi kabisa-laandika Rhein-Neckar-Zeitung.Kunazungumzwa kuipatia mikopo Ugiriki.Katika hali hii laandika gazeti:

"Wenye kuidai Ugiriki, wanabidi kuifutia sehemu ya madeni yao na hapo Ugiriki, itakuwa nchi iliofilisika rasmi na halafu itajenga msingi mpya na imara wa kuiwezesha kusonga mbele.Mpango ilioutangaza Ugiriki hivi sasa wa kubana matumizi,haiwezi kuuepuka.Ugiriki, inapaswa kutupa karata zake zote mezani."

Ama Wiesbadener Kurier kuhusu mzozo huu wa Ugirik,i laandika kwamba, kujitolea kwa hiyari kwa mabenki kuchangia mikopo ili kuiokoa Ugiriki, hata ikiwa itapaswa kuitoza riba ,hii itayatuliza masoko ya fedha na hata kuimarisha msingi wa biashara za mabenki yenyewe....Gazeti laongeza:

Juu ya hivyo, kwa kuwa mabenki nayo yameashiria sasa yatachangia kuisaidia Ugiriki, yanatoa ishara kuwa, hatua zilizopendekezwa ni barabara.Kwahivyo, kiasi gani kitakua mchango wao, ni swali la pili. Kinachohesabika ,ni hatua yenyewe mabenki yaliochukua.

Gazeti la Nord-west-Zeitung, linawataka wasomaji wake humu nchini Ujerumani, kuwaza na kujiweka katika hali waliopo wagiriki wakati huu.Lauliza:

" Wajerumani , wangekuwaje iwapo wangekatiwa nao mishahara yao ,wangepunguziwa pensheni zao , zikapandishiwa bei za vitu na kutozwa kodi zaidi za mapato yao tena kabla ya kupunguziwa thamani ya mapato yao kwa 30% hadi mwisho wa mwaka ?"

Jibu : pengine wangelalamika kama wanavyolalamika sasa wagiriki.Huu ni msiba kwa Ugiriki .Wananchi wake wa kawaida, inawapasa sasa kujitoa mhanga na kufunga mkaja kwa kuwa tu, walifanya uzembe kila mara ,kuwachagua mchanganyiko wa vyama vya kisiasa vilivyodai kuwapigania,wanasiasa,wenye mishahara minono,watumishi wa serikali na mabwanyenye wa kigiriki ambao, wamepora hazina yao tena bila kuona haya wala kujua vibaya."

Mwandishi: Ramadhan Ali/DPA

Uhariri: Abdul-Rahman

No comments:

Post a Comment