KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 11, 2010

Faini Kubwa Sana Kwa Wanawake Wanaovaa Hijab


Wanaume wa kiislamu wa nchini Ufaransa wanaowalazimisha wake zao kuvaa niqab au Burqa (nguo zinazoficha sura zao) watapigwa faini sawa na Tsh. Milioni 26 na kutupwa jela mwaka mmoja.
Adhabu hii ipo kwenye muswada wa kupiga marufuku nguo za kiislamu kwa wanawake zinazoficha sura zao.

Vazi la Niqab na Burqa (Maarufu TZ kama Ninja) litapigwa marufuku nchini Ufaransa kwa kuwa wanasiasa wa Ufaransa wakiongozwa na rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy wanaamini vazi hilo ni la unyanyasaji wa kijinsia na linawanyima uhuru wanawake.

Muswada wa kupiga marufuku mavazi ya kiislamu yanayoficha sura za wanawake utapitishwa kuwa sheria mwezi julai mwaka huu.

Wiki iliyopita nchi ya Ubelgiji ilikuwa nchi ya kwanza ya ulaya kupitisha sheria ya kupiga marufuku Burqa na mavazi mengine ya kiislamu yanayoficha sura za wanawake.

Nchi ya Uholanzi nayo inasemekana iko mbioni kupiga marufuku vazi la Burqa.

Ufaransa mbali ya kupiga marufuku vazi hilo inataka kupitisha sheria ya kuwapiga faini ya Paundi 13,000 (Takribani Tsh. Milioni 26) wanaume wanaowalazimisha wake zao kuvaa mavazi hayo.

Wanawake watakaokamatwa mitaani wakiwa wamevaa mavazi hayo, hawatalazimishwa kuzionyesha sura zao hapo hapo, watapelekwa kituo cha polisi ambapo huko watalazimishwa kuzionyesha sura zao na kupigwa faini ya paundi 130.

Sheria hiyo pia itawabana pia watalii wanaotembelea Ufaransa.

Wanawake matajiri toka nchi za kiarabu watalazimika kuzivua burqa zao wawapo nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment