KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 24, 2010

Busu la Mpenzi Lasababisha Awe Kiziwi


Mwanamke mmoja wa nchini China amekuwa kiziwi sikio moja baada ya kupewa mabusu ya nguvu ya kunyonyana ndimi na mpenzi wake. Vyombo vya habari nchini humo vimekuwa vikiwaonya vijana kupunguza kupeana mabusu ili kuepuka madhara kama hayo yasitokee tena.
Mwanamke huyo anayekisiwa kuwa na umri wa miaka 20 na ushee wa mji wa Zhuhai kwenye jimbo la Guangdong alienda hospitali akiwa hasikii chochote kupitia sikio lake la kushoto, yameripoti magazeti ya China.

Tukio hilo lilitokea baada ya mwanamke huyo kupeana mabusu ya nguvu ya kunyonyana ndimi na mpenzi wake kwa muda mrefu.

Baada ya tukio hilo, makala mbalimbali zimeandikwa kwenye magazeti ya China vijana wakionywa wapunguze tabia ya kunyonyana ndimi sana kuliko kawaida.

"Kunyonyana ndimi kwa kawaida hakuna madhara lakini watu inabidi wawe waangalifu kidogo", liliandika gazeti la China Daily.

"Wakati wa kunyonyana ndimi, presha toka kinywani huisukuma ngoma ya sikio nje na hivyo kusababisha sikio kupoteza usikivu wake" alisema daktari aliyemtibia msichana huyo alipokuwa akitoa maelezo sababu ya msichana huyo kuwa kiziwi sikio moja.

Maelezo zaidi kuhusiana na madhara ya mabusu ya kunyonyana ndimi yaliandikwa kwenye gazeti la Shanghai Daily, ambalo liliandika: "Busu la nguvu husababisha uwiano wa msukumo wa hewa ndani ya masikio kuharibika na hivyo kusabisha ngoma ya sikio kupasuka".

Madaktari wamesema kuwa mwanamke huyo aliyepoteza usikivu sikio moja ataweza kusikia tena kupitia sikio hilo baada ya miezi miwili.

No comments:

Post a Comment