KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 24, 2010

Burundi kupiga kura za madiwani


Kulingana na mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, usiku wa kuamkia Jumatatu radio za nchini zilikuwa zikitangaza juu ya Tume ya Uchaguzi nchini kushindwa kuwasilisha vifaa vya upigaji kura katika vituo vingi.

Radio hizi zimenulikiwa zikisema kuwa upungufu mkubwa umekuwa makaratasi ya kupigia kura. Hata hivyo maafisa wa tume hiyo waliahidi kuwa kufikia leo asubuhi watakuwa wamekamilisha yote yanayohitajika.

Afisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo jana ilisaidia tume hiyo ya uchaguzi kwa kuwasilisha masanduku ya kupiga kura katika maeneo ya mbali kwa kutumia helikopta zao. Sehemu kubwa ya Burundi ina milima na barabara ni mbovu.

Muda unapokaribia wa kupiga kura tayari propaganda zinaendelea kuenea. Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali umesema kuwa habari zisizothibitika zimeonyesha kuwa chama kimoja cha kisiasa nchini humu zimewapa wafuasi wao bunduki.

No comments:

Post a Comment