KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, April 27, 2010

Wanamaji wa Urusi sio tatizo Ukraine


Bunge la Ukraine limepitisha hatua ya Urusi kuendelea na shughuli zake katika kituo cha jeshi la wanamaji cha Crimea, katika maji ya Black Sea.

Hata hivyo kulikuwa na fujo bungeni wakati wa majadiliano kuhusu hatua hiyo.

Wabunge walipigana, huku Spika akijificha chini ya mwavuli, wakati wabunge walikuwa wakimpiga kwa mayai.

Mabomu yanayotoa moshi pia yalitegwa nje ya bunge.

Nje ya bunge, polisi walipambana na maelfu ya waandamanaji, wengine wakiunga au kupinga makubaliano ya wiki iliyopita kati ya marais wa Ukraine na Urusi ya kuongoza muda zaidi katika Urusi kukimiliki kituo hicho cha kijeshi.

No comments:

Post a Comment