KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, April 27, 2010

Somaliland:Wahandisi walalamikia ukosefu wa kazi

Wahandisi kutoka nyanja mbali mbali katika eneo lililojitangazia uhuru la Somaliland, wamebuni chama kitakachotetea maslahi yao.

Mmoja wa viongozi wa chama hicho, Hussein Sheikh Adam, amesema madhumuni makuu ya chama hicho ni kuzuia wahandishi kutoka mataifa ya kigeni kuchukua nafasi zao za kazi.

Idadi kubwa ya watu tajiri katika eneo hilo na mashirika ya kutoa ajira, wamekuwa wakiwaajiri wahandisi kutoka nchi jirani ya Kenya kusimamia shughuli za ujenzi wa nyumba na viwanda.

Wahandisi hao ambao wameghathabishwa na kitendo hicho wanasema wao wanatajiriba ya kutekeleza kazi hiyo inayofanywa na wahandisi kutoka nchi za kigeni.

No comments:

Post a Comment