KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

Waziri wa zamani wa Somalia mashakani Marekani


Waziri wa zamani wa Somalia mashakani Marekani

Raia kadhaa wa Kisomali ambao walisema walikuwa waathiriwa wa mateso wametoa wito kwa Mahakama Kuu nchini Marekani kuwaruhusu kumchukulia hatua za kisheria aliyekuwa makamu wa rais na waziri ulinzi wa Somalia anayeishi Marekani.
Marshal Mohamed Ali Samantar, alikuwa makamu wa rais na waziri wa ulinzi mnamo miaka ya thamanini.

Jaribio la kumshitaki limeanzishwa chini ya sheria za Marekani, zinazoruhusu kesi kuhusu mateso yalitokea nje ya nchi kuweza kusikilizwa, ikiwa nchi ambako uhalifu ulitendeka haiwezi kushughulikia kesi hizo.

Waandishi wa habari wanasema Bw Samantar anadai kuwa na kinga kama afisa wa zamani wa serikali.

Majaji nchini Marekani wameonekana kuwa waangalifu katika matamshi yao ikiwa anaweza kufunguliwa mashtaka nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment