KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

Nigeria yachunguza mauaji ya abiria


Bunge la Senate nchini Nigeria limeanzisha uchunguzi kuhusu picha zinazoonyesha miili ya waathiriwa wa kisa cha wizi wa mabavu kwenye barabara kuu ya Lagos kuelekea mjini Benin.
Picha hizo zimesambazwa kwenye mtandao na zinaonyesha maiti zimetapakaa barabarani na maandishi yanayosema abiria hao waliamriwa kutoka kwenye basi na kulala chini.

Wanawake walibakwa kisha dereva wa basi hilo akiamuriwa kuwakanyanga abiria wake mara kadhaa.

Mkuu wa Polisi ametakiwa kufika mbele ya bunge la Senate kutoa maelezo juu ya hali ya usalama katika barabara za nchi hiyo.

Visa kama hivi ni vya kawaida nchini humu na abiria ambao wametekwa hulazimishwa kulala chini na kuporwa.

Mara nyingi abiria hao hugongwa na malori ambayo yanaendeshwa kwa kasi kwenye barabara hizo.

No comments:

Post a Comment