KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

Waliokufa maporomoko Uganda wazikwa


Waliokufa maporomoko Uganda wazikwa

Maziko yamefanyika nchini Uganda kwa watu waliouawa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyokumba vijiji vitatu karibu na mji wa Bududa.
Mwandishi wa BBC Joshua Mmali akiwa eneo yalipotokea maporomoko hayo kwenye miteremko ya mlima Elgon amesema katika baadhi ya sehemu familia nzima imezikwa.

Kiasi cha maiti 90 zimekwishapatikana na zaidi ya watu 260 bado hawajulikani walipo.

Umoja wa Mataifa umesema unapeleka mahema kwa watu wanaofikia 5,000 ambao nyumba zao zimezolewa na maporomoko hayo.

Katika kijiji kimoja watu walioshuhudia wamesema wanafunzi wa shule walikuwa wamejibanza katika zahanati na baadae ikasombwa na maporomoko hayo.

No comments:

Post a Comment