KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

MONUC yajadili kuondoa wanajeshi DRC


MONUC yajadili kuondoa wanajeshi DRC

Umoja wa Mataifa umesema umeanzisha majadiliano na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuhusu kuondolewa kwa awamu vikosi vya kulinda amani.
Harakati za Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Congo, MONUC, ndiyo yenye idadi kubwa ya wanajeshi wanaolinda amani katika maeneo yote amabayo Umoja wa Mataifa hulinda amani duniani.

Muda wa vikosi hivyo unatarajiwa kumalizika mwezi Mei.

Tangazo hilo lilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anayeshughulikia harakati za kulinda amani, Alain Le Roy, baada ya kukutana na Rais Joseph Kabila.

Hakuna ufafanuzi uliotolewa kuhusu tarehe ambapo wanajeshi hao wataanza kuondolewa, lakini serikali ya Congo inataka waondolewe mwaka huu.

Bw Le Roy alisema kundi la Umoja wa Mataifa lilipatiwa muda wa mwezi mmoja kutathmini jinsi walinda amani hao watakavyoweza kuanza kuondoka Congo kabla ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili kuongezewa muda kwa MONUC, mwezi Juni.

Msemaji wa serikali ya Congo, Lambert Mende, amesema askari wa kulinda usalama wa Umoja wa Mataifa wanapaswa kuondoka nchini humo isipokuwa mkoa wa mashariki wa Kivu ifikapo mwisho wa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment