KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, February 1, 2010

Viongozi wa muungano wa Afrika

Viongozi wa muungano wa Afrika, AU, walikatiza tamaa ya kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi ya kupata muda wa ziada kama mwenyekiti wa muungano.

Badala yake walimchangua Rais Mbingu wa Mutharika wa Malawi.

Hadi dakika ya mwisho, kulikuwa na wasiwasi kwamba Gaddafi hangekubali kuondoka.

Katika hotuba yake ya mwisho, alimtakia heri njema Rais Mutharika.

Hata hivyo alilalamika kwamba hakuhusishwa vilivyo kama kiongozi wa AU kuwakilisha bara Afrika kwenye mikutano muhimu kama ile ya maataifa tajiri duniani G8.

Rais Mutharika alishangiliwa mno na viongozi wenzake huku akiahidi kulipa uzito swala la bara Afrika kuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula

No comments:

Post a Comment