KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, February 4, 2010

Libya yaonywa kuhusu kuziba wavuti

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeionya, Libya kuacha kuzuia wavuti za upinzani na kurasa za tovuti kama vile YouTube zisionekane.
Wanaharakati wamesema Tripoli ilianza kuchukua hatua kali za kinidhamu tarehe 24 Januari, ikizuia wavuti kadhaa za kigeni zinazoripoti kuhusu Libya zisionekane, na wavuti nzima ya YouTube.

Shirika hilo limesema katika taarifa yake, "Serikali inarudi katika enzi zake za kudhibiti vyombo vya habari".

Mwezi Desemba, shirika hilo liliisifia Libya kwa kuwaruhusu waandishi wa habari kufanya kazi nchini humo.

Lakini wamesema hatua yao ya hivi karibuni inaanza kuleta wasiwasi hasa katika uhuru wa habari.

No comments:

Post a Comment