KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 6, 2010

Uchaguzi wa Gavana unaendelea Anambra
Wapiga kura katika jimbo la Kusini Mashariki mwa Nigeria, la Anambra wanaendelea na shughuli ya kupiga kura hii leo kumchagua gavana mpya wa jimbo hilo.
Upigaji kura huo unaonekana kama mtihani kwa uwezo wa nchi hiyo, kufanya uchaguzi wake mkuu kwa njia ya haki na huru mwaka ujao. Wagombea 25 wanawania kiti hicho ambacho kwa sasa kinashikiliwa na upinzani.

Maelfu ya polisi wa ziada wanashika doria katika jimbo hilo, ambalo lina historia ya wizi wa kura.

Uchaguzi huu unafanyika wakati Rais wa nchi hiyo, Umaru Yar'Adua, kwa mwezi wa tatu sasa yuko hospitalini nchini Saudi Arabia, na kutokuwepo kwake kumesababisha msukosuko wa kisiasa nchini humo.

No comments:

Post a Comment