KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, February 9, 2010

Mbinyo wa kimataifa kwa ajili ya vikwazo vipya dhidi ya Iran umeongezeka


Vikwazo vikali zaidi.

Washington.

Mbinyo wa kimataifa kwa ajili ya vikwazo vipya dhidi ya Iran umeongezeka jana Jumatatu baada ya Iran kutangaza mipango ya kurutubisha kwa kiwango cha juu madini ya uranium na kuongeza maeneo mapya kumi ya kinuklia , na kuongeza hofu ya mataifa ya magharibi kuwa inataka kutengeneza bomu la kinuklia. Marekani na Ufaransa zimeongoza miito katika kile ambacho kinaweza kuwa sehemu ya nne ya vikwazo vikali zaidi, wakati wabunge waandamizi nchini Urusi, nchi ambayo hapo zamani ilikuwa inahimiza mazungumzo zaidi badala ya adhabu, imesema kuwa hatua za kiuchumi ni lazima zifikiriwe. Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema kuwa maslahi ya Iran yatahifadhika iwapo haitakuwa na silaha za kinuklia.

Balozi wa Iran katika umoja wa mataifa mjini Vienna amekanusha madai kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa na hofu kuhusiana na urutubishaji huo wa kiwango cha juu wa madini ya uranium ambayo nchi yake inapanga kufanya.

No comments:

Post a Comment