KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 20, 2010

Wanajeshi wa Marekani wameongeza oparesheni zao nchini Haiti kuimarisha usalama


Marekani yaongeza oparesheni Haiti

Wanajeshi wa Marekani wameongeza oparesheni zao nchini Haiti kuimarisha usalama na usambazaji wa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi.

Jeshi hilo limesema kuwa uwanja wa ndege nchini humo unahudumia zaidi ya ndege mia moja themanini kwa siku.

Pentagon imesema kuwa inaandaa sasa viwanja viwili zaidi ili kupunguza msongamano katika uwanja huo.


Wakati uo huo baraza la usalama la umoja wa mataifa limeamua kutuma wanajeshi 3,500 zaidi wa kulinda amani ili kusaidia katika usambazaji wa misaada.

No comments:

Post a Comment