KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 20, 2010

Takriban watu miamoja arobaini na tisa wamefariki kwenye ghasia kati ya makundi ya kikristo na kiisilamu katika mji wa Jos


Ghasia za kidini zakithiri Nigeria

Takriban watu miamoja arobaini na tisa wamefariki kwenye ghasia kati ya makundi ya kikristo na kiisilamu katika mji wa Jos kwa mujibu wa maafisa wa utawala.

Viongozi wa kidini na wahubiri waliwafahamisha waandishi wa habari kuwa maiti za waliokufa zitazikwa katika kaburi la pamoja.

Idadi kamili ya waliofariki ingali kujulikana.

Makamu wa rais wa Nigeria Good Luck Jonathan ameagiza kutumwa kwa wanajeshi zaidi katika mji huo kudhibiti usalama.

Pia ametuma maafisa wakuu wa ujasusi kuchunguza zaidi ripoti kuwa mapigano hayo huenda yamesambaa katika miji mingine jirani.

No comments:

Post a Comment