KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 20, 2010

Sudan kukubali kusini ijitenge?
Rais Omar al-Bashir amesema atakubali upande wa kusini ujitenge iwapo raia wa eneo hilo watapiga kura ya maoni ya kutaka uhuru wao mwakani.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka mitano tangu kumalizika kwa vita vya pande mbili za kusini na kaskazini, chama chake cha Northern Congress hakikutaka kusini ijitenge.

Lakini amesema chama hicho kitakuwa cha kwanza kukubaliana na uamuzi huo.

Wachambuzi wamesema Bw Bashir ametumia lugha isiyo ya kawaida, yenye kuonyesha kuridhia ambayo imepokelewa vyema.

Katika miezi ya hivi karibuni wasiwasi umekuwa ukiongezeka baina ya pande hizo mbili.

No comments:

Post a Comment