KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 30, 2010

Sodo zawasaidia wanafunzi, Ghana


Sodo zawasaidia wanafunzi, Ghana

Idadi ya wanafunzi wa kike wasiohudhuria shule nchini Ghana inaweza kupungua kufikia nusu kwa kugawa sodo, 'sanitary towels' bure.
Utafiti uliofanywa na chuo cha Oxford kwa miezi sita umegundua, mabinti walijiamini zaidi kuhudhuria shule baada ya kutumia sodo na kuelimishwa juu ya usafi.

Utafiti huo ulifanywa katika vijiji vinne ambapo njia za kiasili zilizokuwa zikitumika wakati mabinti hao wakiwa kwenye hedhi ni vitambaa.

Mtafiti Linda Scott amesema, "Ni mwiko kuzungumzia masuala hayo, lakini tumegundua kuwa walikua na hamu ya kujaribu kitu kipya."

Ameiambia BBC, "hawa mabinti ni maskini kiasi ambacho wanatakiwa kutumia kitambaa chochote watakachokuwa nacho."

No comments:

Post a Comment