KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 20, 2010

Katika kile kinachoonekana kuwa pigo kubwa kwa utawala wa Rais Obama


Republican yanyakua Massachusettes

Katika kile kinachoonekana kuwa pigo kubwa kwa utawala wa Rais Obama, Scott Brown wa chama cha Republicans ameshinda uchaguzi wa seneta katika jimbo la Massachusettes nchini Marekani.

Licha ya kuwa Obama mwenyewe alimfanyia kampeini mgombea wa democrats Martha Coakly, bado chama hicho kilipoteza kwa idadi ndogo ya kura. Matokeo haya yatafanya kampeini ya Rais Obama ya kupitisha mswada wa mabadliko katika huduma ya afya nchini humo kuwa ngumu zaidi.

Uchaguzi huo mdogo unafuatia kifo cha aliyekuwa seneta wa jimbo hilo mwaka jana Edward Kennedy, mwanasiasa mkongwe wa Democrats aliyeshikilia kiti hicho kwa takriban miaka hamsini.

No comments:

Post a Comment